Breaking News..Mzee Akilimali Ajitokeza Kuwania Uenyekiti wa Yanga..

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache zilizopotia.

Lakini pia maamuzi hayo ya Manji yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.

Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.

Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.

“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.

“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.

“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,” alisema Akilimali.

Facebook Comments

Maamuzi ya BUNGE kuhusu waliohusika Kusaini Mikataba Mibovu Ya Madini

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.

“Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla,” amesema Mkuchika.

Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.

Facebook Comments

SHINYANGA: Binti wa miaka(24) amefariki dunia kwa kujikata koromeo kwa chupa ya soda.

Mkazi wa Mtaa wa Mabambase katika Manispaa ya Shinyanga, Saada Elias(24) amefariki dunia kwa kujikata koromeo kwa chupa ya soda.

Mwanamke huyo alijiua kwa chupa muda mfupi baada ya kunyang’anywa kisu wakati akijaribu kujichinja kwa madai ya kuandamamwa na ugumu wa maisha.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa tisa usiku, wakati Mwanamke huyo akiwa chumbani kwake alikokuwa amelala na mdogo wake wa miaka 12 na mtoto wake wa miaka minne.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alichukua uamuzi wa kujichinja kwa kisu lakini mdogo wake huyo alishituka kutoka usingizini na kumpokonya silaha hiyo ndipo alipochukua chupa ya soda na kujikata koromeo papo hapo.

Akisimulia tukio hilo, Peter Maduhu ambaye ni mpangaji mwenzake alisema baada ya mdogo wake kuomba msaada kuwa dada yake amejichinja ndipo alipoamka na kutoa msaada lakini walipoingia ndani walimkuta tayari ameshajikata koromeo kwa kutumia kipande cha chupa ya soda.

Alisema kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akilalamiaka kuwa anaumwa kwa muda mrefu ugonjwa ambao hakua akiutaja.

Aidha alisema marrehemu alikuwa akidai kuwa hakuna ndugu wala mtu wa kumsaidia licha ya kuandamawa na ugumu wa maisha.

”Marehemu alikuwa akifanya biashara ya Mama ntilie” alisema Maduhu ”lakini siku ambayo alikuwa akitaka kujiua mdogo wake alikuwa akisema Dada yao yupo kazini”

”Kumbe amejifungia ndani na ilipofika majira hayo ya saa tisa usiku ndipo tukasikia kelele za mtu akiomba msaada na tulipofika chumbani kwake alikuwa amejikata koromeo.

Baba mzazi wa marehemu Elias Ruleja ambaye ni mkazi wa mkoani Kagera alisema mtoto wake huyo alitoroka nyumbani mwaka jana kuja kuishi Shinyanga bila ya yeye kufahamu hadi alipopokea habari za kifo chake. Alisema amahuzunishwa sana na kifo hicho huyo akiwa mtoto peke aliyekuwa amebaki baada ya kaka yake kufariki miaka mingi iliyopita.

Nipashe

Facebook Comments

Video: Rais Alivyokutana na kuzungumza na wamiliki wa ACACIA.. TAZAMA HAPA

Rais John Pombe Magufuli (JPM) amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni mama ya uchimbaji wa madini ya Barrick Canada, Profesa John Thornton na kufanya naye mazungumzo Ikulu leo.

Amesema Barrick imepitia mapendekezo yote ya kamati ya pili ya mchanga wa madini na kuwa imekubali kulipa chochote ambacho kitaonekana wanatakiwa kulipa.

“Baada ya kuwaona nilifurahi na nikasema hawa ni wanaume, wakasema yaliyotokea ni bahati mbaya na wanatubu kwa hayo.” Amesema

Rais amesema baadaye Barrick watakuja na timu yao ya wanasheria wakati kwa upande wa Tanzania nao itakuwepo timu ya wanasheria wakiongozwa na Profesa Palamagamba Kabudi.

“Itakuwa ni timu ya maprofesa kwa maprofesa,” amesema.

Amesema timu hiyo ya Barrick ilipitia mapendekezo yote na wakakubali kuwa wapo tayari kulipa baada ya majadiliano na makubaliano yatakayoafikiwa.

Facebook Comments

MPYA Muda huu Kutoka kwa Rais wa TLS Mhe Tundu Lissu, SOMA HAPA

Rais wa Chama cha wanasheria Tanzania (TLS) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mheshimiwa Tundu Lissu amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikungi na kuwataka polisi kuacha kutekeleza maagizo ya baadhi ya viongozi wa siasa kutoa amri ya maneno ya kuwa kamata watu bila ya kuwa na kibali halisi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kati Bi.Aisha Luja amemuomba Mheshimiwa Tundu Lisu kundelea kusimamia mikataba ya madini ambayo imekuwa ikitekelezwa kisiasa na kunyimwa kwa uhuru wa vyombo vya habari,huku Mbunge wa Kilombero Mheshimiwa Peter Ambrosi Jualikali akiwataka wananchi wa Jimbo la Singida Mshariki kumtumia vizuri mbunge wao Tundu Lisu.

Mheshimia Tundu Lisu baada ya kufika katika mkutano huo akiwa na badhi ya wabunge wa CHADEMA,uliohudhuriwa na wananchi wengi kutoka katika vitongoji vya Jimbo la Singida mashariki alivishwa mavazi ya asili ikiwa ni ishara ya shujaa

Facebook Comments

UBUYU MPYA : Mobeto Achekelea VITA ya Diamond na Zari, Hiki Ndicho Alichopost muda HUU..

Ugomvi haukuishia hapo, Mobeto nae aliendeleza vita yake chini kwa chini, ambapo siku moja aliwahi kupost picha akiwa chumba cha hoteli ambacho Diamond nae kwa wakati wake aliwahi kupost akiwa kwenye chumba hicho (Maana yake kuwa siku hiyo alilala chumba hicho na Diamond) Picha hii Hapa Chini

Mobeto hakuishia hapo kurevenge matusi aliyotukanwa na Zari, siku nyingine Alipost Picha akiwa amevaa nguo za Diamond.

Sasa baada ya timbwili la leo, kati ya Zari na Diamond ambapo wametukanana matusi Instagram kisha baada ya Muda wakafuta post zao, Mrembo Hamisa Mobeto ambaye Inasemekana ana Mimba ya Diamond Sasa hivi (Na ambaye anapendwa na Mama Diamond) inaonekana amefurahia timbwili hilo maana linamsafishia njia ya kuwa na Diamond, Kupitia Account yake ya Instagram akiwa ameficha ‘Kibendi chake’ Ameandika “It Might Take A Year

Facebook Comments

KIMENUKA : Zari AMPOROMOSHEA MATUSI DIAMOND…. SOMA HAPA

Diamond aliandika “(the reason why sometimes i prefer being a player than a committed loyal man….👍) Ndiomaana wakati mwingine naonaga bora tu nile na kusepa…. maana hawathaminikagi wala kuaminika hawa….👍” Bila kuchelewa Baada ya Diamond Platnumz kupost hiyo, Zari naye alijibu kwa Matusi “And to the fools circulating this nonsense mnitole nja zakisenge kwa maisha yangu punda nyinyi…..”. Hicho ndio kinachoendelea Instagram kama huna Instagram tutakuletea hapa hapa tifu hili, Una Maoni gani?

Facebook Comments

KITUKO Kingine cha WABUNGE Leo BUNGENI

Bunge limezizima kwa makofi baada ya hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.Wabunge wa upinzani ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Wabunge wamesimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.

“Tuna imani na Mkaaapa…oya oya oya
Mkapa kweeeli…kweli
Kweli, kweli, kweli Mkapa.

Tuna imani na Kikweeetee…oya oya oya
Kikwete kweeli
Kweli, kweli, kweli Kikwete.”

Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.

Facebook Comments

ACACIA wapinga vikali Matokeo ya Kamati ya pili ya Rais MAGUFULI

Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais

Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.

Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia

Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku ya kuuza nje.

Acacia inakanusha vikali tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya kimataifa vinavyoendana na IFRS.

Acacia kwa muda mrefu tulitaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo, ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya nchi hadi sasa.

Acacia bado inakaribisha mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti YAO
www.acaciamining.com

Facebook Comments