Uncategorized

Facebook yaachia App ya ‘Messenger Kids’ Maalumu kwa Matumizi ya Watoto

By  | 

Mtandao wa Facebook umeachia App yake ya ‘Messenger Kids’ Maalumu kwa matumizi ya watoto waliochini ya miaka 13 kutumia kwa kuchati na watoto wenzao.

App hiyo ya ‘Messenger Kids’ imeundwa sawa na mfumo wa Messenger ambao hutumiwa na watumiaji wa Facebook kutuma na kupokea meseji.

Messenger Kids inatarajiwa kuongeza ufahamu wa watoto kuhusu matumizi ya Facebook na hivyo kuongeza ukaribu na wazazi wao pindi wanapokuwa mbali .

Kwenye App hiyo kuna sticker zenye maadili ambazo ni maalumu kwa watoto na ili mtoto wako aanze kutumia mzazi ni lazima uipakue App hiyo kwenye Play Store au iStore bure.

Mpaka sasa imeelezwa kuwa App hiyo huenda ikapata changamoto kubwa kwa kuingiliwa na watu wakubwa wanaodanganya umri ambapo Facebook wamekiri kuwa zaidi ya watoto milioni 20 waliochini ya miaka 13 wanatumia mtandao huo.