Thursday, July 17, 2025

Watu 7 wapoteza maisha ajali ya ambulance na toyo wilayani Mafinga

Share

Watu saba wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali ya gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kugongana na toyo katika eneo la Luganga, lililopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi wa ajali hiyo leo Jumamosi, Aprili 19, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Linda Salekwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

Amesema kuwa taarifa zinaonyesha watu hao walikuwa wanakwenda shambani kufanya kazi, ndipo gari hilo likagongana na toyo hiyo na kusababisha watu hao kufariki dunia na wengine kujeruhiwa

Table of contents [hide]

Read more

Local News