Wednesday, July 16, 2025

Rais Samia kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika

Share

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 17 Julai 2025. Mkutano huo utafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Mgeni Rasmi aliyealikwa kufungua mkutano huo wa kimataifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amealikwa kushiriki kwa nafasi ya Mgeni Maalum wa mkutano huo kushuhudia Tuzo mahsusi za Miaka thelethini (30) ya Baraza la Habari Tanzania.

Mgeni mwingine mashuhuri ni Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Dkt. Tawfik Jelassi; huku tukitarajia baadhi ya mawaziri wa sekta ya habari na mawasiliano kutoka katika mataifa ya Afrika kuhudhuriaMawaziri hao ni pamoja na Mhe. William Kabogo Gitau, Waziri wa Habari na Uchumi wa Kidijitali, Kenya, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania.

Mkutano huu unaandaliwa kwa mara ya kwanza na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (Network of Independent Media Councils of Africa—NIMCA), Umoja wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (East Africa Press Councils-EAPC), na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama mshirika mahususi.

Aidha, mikutano mingine ya kimataifa itafanyika sambamba na mkutano huo, kama vile, mkutano wa East Africa Press Councils (EAPC), na World Association of Press Councils (WAPC).

Watu zaidi ya 500 (mia tano) wanatarajiwa kushiriki ambapo 150 (mia moja Hamsini) watatoka nchi mbalimbali duniani. Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu: “Advancing Media and Communication Regulations for Journalism Excellence in Africa

Table of contents [hide]

Read more

Local News