Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredy Lowassa amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake cha CCM kutetea nafasi yake ya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025 nchini
Fredy ambaye alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, amekuwa mtangaza nia wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu hiyo baada ya zoezi la uchukuaji fomu kufunguliwa rasmi kufuatia kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, katikati ya wiki hii