Thursday, July 17, 2025

Sio Fiston tena, sasa ni Mahmoud Mayele, baada ya kubadili dini

Share

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambae kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele amebadilisha dini kutoka kuwa Mkristo na sasa ni Muislamu

Ripoti za mitandao zinaeleza kuwa Mayele amebadilisha dini miezi sita iliyopita na hata kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan alikuwa akijumuika na wenzake waliofunga mfungo huo ambao ni moja ya nguzo tano za dini ya kiislamu

Uamuzi wa Mayele kubadili dini ulichagizwa na wachezaji wenzake wa Pyramids FC, haswa Ramadan Sobhi na Karim Hafez, na inaripotiwa kuwa maamuzi hayo aliyafikia kipindi cha mwezi wa Ramadhani.

Baada ya kubadilisha dini kwa sasa Mayele hatambuliki kama Fiston Mayele bali amechagua jina la Mahmoud na hivyo anaitwa Mahmoud Mayele.

Table of contents [hide]

Read more

Local News