Simba SC yatanguliza mguu mmoja nusu fainali kombe la Shirikisho

Goli pekee la Jean Charles Ahoua katika dakika ya 45+2 kwenye Uwanja wa Amaan, limeiwezesha Simba kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Stellenbosch, katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika

Licha ya ushindi, Wachezaji wa Simba wamekosa nafasi kadhaa za wazi katika mtanange huo, hivyo mchezo wa marudio unatarajiwa kupigwa Aprili 27, 2025 kwenye Dimba la Moses Mabhida, Durban, Afrika Kusini

Mshindi baina ya pande hizo anatarajiwa kukutana na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Exit mobile version