Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo April 21,2025 kwenye Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88.
Vatican imethibitisha kifo cha kiongozo huyo wa kanisa ambaye atakumbukwa kama kiongozi wa mageuzi wa Kanisa Katoliki ambaye alitaka kufanya vipaumbele vya uchungaji na umma vya Vatikani kuwa vya kisasa,
Papa Francis, ambaye alikuwa papa wa kwanza kuzaliwa au kukulia nje ya Ulaya katika karne 12, wa kwanza kutoka Amerika na Mjesuti wa kwanza kushika nafasi hiyo amefariki akiwa kwenye makazi yake Vatican na taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa.
Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye afya yake kuimarika.