By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: Ofisi ya Makamu wa Rais yapongezwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Kitaifa

Ofisi ya Makamu wa Rais yapongezwa

Mwandishi Wetu
Last updated: March 20, 2025 9:51 am
Mwandishi Wetu
2 months ago
Share
SHARE

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ubunifu mkubwa unaobeba uhalisia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Pongezi hizo zimetolewa Machi 18, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Dkt. Joseph Mhagama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2024/2025 na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2025/2026.

Dkt. Mhagama amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ofisi ya mfano kwa sasa kutokana na kufanya kazi nzuri kutokana na watendaji wake kutekeleza maelekezo mbalimbali ya kamati na hivyo kuweza kupata matokeo makubwa katika kipindi kifupi.

“Wajumbe wa kamati hii tupo kwa zaidi ya miaka 10 sasa, lakini kwa kipindi hiki kifupi tumeshuhudia mageuzi makubwa ya kiutendaji katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi hii, tunaomba tuendelee kushirikiana ili kufikia malengo” alisema Mhagama.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameishukuru kamati hiyo kwa ushirikiano unaoendelea kuipatia ofisi hiyo na hivyo pongezi hizo zitakuwa chachu ya kufanya kazi nzuri zaidi.

“Hii ni kamati kubwa sana, kupokea pongezi hizi si jambo jepesi….hii inatupa faraja kuwa tunachokifanya kinaonekana na tuna ahidi kuongeza juhudi katika kutekeleza maelekezo mbalimbali yanayotolewa,” alisema Masauni.

Aidha Mhe. Masauni amesema Ofisi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia ushauri na maoni ya kamati hiyo ili kufikia malengo iliyojiwekea.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Daraja la Magufuli kuanza kutumika Aprili 30

Uzinduzi wa jengo la hazina Mkoani Geita

RC Dar: Usalama Dar ni shwari, Ujenzi Jangwani mboini kuanza

Serikali yazidi kuimarisha imarisha huduma za fedha ikizundua jengo la Hazina Ndogo Geita

Mbunifu wa jina la TANZANIA afariki dunia akiwa Uingereza

TAGGED:BungeMakamu wa RaisMasauni
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Kamati ya Bunge yakoshwa na utendaji TPA
Next Article Umeme kila mahali ni ndoto ya Rais Samia
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version