Kikosi cha Stellenbosch kimetua nchini tayari kwa pambano la kwanza la nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba, huku ikipata pigo baada ya straika nyota wa timu hiyo ya Afrika Kusini kuumia na kumfanya kocha Steve Barker kukuna kichwa mapemaa.
.
Kocha huyo, amekiri kikosi chake kimeifuata Simba kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar bila ya mshambuliaji muhimu, Ashley Cupido aliyeumia mapema wiki hii katika mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
.
“Ndio inaonekana kam ni msuli mbaya wa paja, hakuna uwezekano wa kupatikana katika mchezo huo. Tutafanya tathmini zaidi kujua ukubwa wa jeraha lake. Kiuhalisia majeraha hayo yanapotokea mchezaji anakuwa nje hadi wiki sita.
.
“Bahati mbaya kwake, pia ni bahati mbaya kwetu, ukizingatia kuwa Bradley Mojela bado yupo nje na sasa Ashley, ni dhahiri sio taarifa nzuri, lakini lazima tutafute suluhu.”
.
Kutokana na hali hiyo, kocha Barker anazidi kuumiza kichwa kwani winga wake, Langelihle Phili anatakiwa kujiunga na kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini chini ya miaka 20 kwa ajili ya kushiriki Afcon U20 nchini Misri, hivyo kuna uwezekano naye kumkosa.
.
Akizungumzia ishu ya Phili, Barker amesema “Anatakiwa kuripoti kambini Jumapili, lakini tutamwomba asafiri nasi na kuripoti kambini siku ya Jumatatu ambayo tutakuwa tumerudi baada ya kutoka Tanzania. Kwa kuwa Ashley hayupo, tungeomba (Phili) aje kwa ajili ya mechi hiyo.”
Stellenbosch kuwakosa wakali wawili ikiivaa Simba kombe la Shirikisho

Leave a Comment