By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: DKT. BITEKO: Wakristo liombeeni Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Kitaifa

DKT. BITEKO: Wakristo liombeeni Taifa

Mwandishi Wetu
Last updated: April 20, 2025 7:22 pm
Mwandishi Wetu
4 weeks ago
Share
SHARE

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa wakristo kuliombea Taifa amani, utulivu, umoja na mshikamano uendelee ikiwa ni kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 20, 2025 jijini Mwanza wakati aliposhiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la African Inland Church (AIC) – Makongoro.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi na una michakato mbalimbali ya kujiandikisha, kugombea, kupiga kura na kutangaza matokeo. Kwa niaba ya Serikali napenda kuwaomba waumini wa AICT na wale ambao tunadhani tuna uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali tujitokeze kwa wingi tugombee, wale tu wenye nia ya kweli tuhakikishe tunawasaidia watu katika hali zao,” amesema Dkt. Biteko.

Sambamba na kugombea amewahimiza waumini kuliombea Taifa kuelekea wakati na baada ya uchaguzi “ Tujitokeze ili tuweze kugombea kwa ajili ya kuhudumia nchi yetu na wakati wa kampeni utakapofika naomba tuendelee kuliombea Taifa,”

Ameongeza kuwa Mwl. Julius Nyerere na viongozi wengine waliweka misingi imara ya amani na kushikamana wakati wote na Tanzania inafahamika duniani kote kama kisiwa cha amani hivyo waumini hao waliombee Taifa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya katika Taifa na kuendelea kufanya nchi kuwa na amani.

Amebainisha “Tuliyofundishwa kwenye ibada ya leo ni pamoja na kuwa ilikuwa kusudi la Mungu kwa Yesu afufuke na tunamshukuru Mungu kwa ajili ya siku ya leo ya kutufanya kuwa hai na sisi waumini wa Kanisa hili kukutana hapa na kuabudu kwa pamoja,”

Pamoja na hayo Dkt. Biteko amewaeleza waumini wa Kanisa hilo kuwa kufufuka kwa Yesu ni ishara ya ushindi na kuwa wote wameshinda pamoja na Yesu kama alivyoshinda mauti, watashinda pia katika kukamilisha ujenzi wa Kanisa lao ambalo wanaendelea kulijenga.

Waumini wa kanisa la AICT wakimsikiliza Dkt. Biteko

Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Musa Masanja Magwesela amesema waumini hao watumie nafasi ya kufufuka kwa Yesu kwa kuleta mabadiliko katika maisha yao.

Awali akihubiri katika ibada hiyo, Mchungaji wa Kanisa la African Inland Church kutoka Turkana nchini Kenya, Stephen Kilel amesema kuwa tukio la Yesu kufufuka ni tukio kuu linalowapa ujasiri wa kujua imani yao ni thabiti.

“Wapo watu wengine ambao hawaamini kama Yesu amefufuka. Sisi tunaweza kupata matumaini makubwa kumbe maisha yetu hayaishi pale ambapo kifo cha mwili kimetupata, kuna ufufuo ambao unatupa nguvu ya kuzungumza juu ya habari njema,” amesema Mchungaji Kilel.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Sita wafariki dunia ajali ya basi na lori Dodoma

Daraja la Magufuli kuanza kutumika Aprili 30

Mahakama ya Rufaa yabariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa SSP Bageni

Polisi Simiyu watoa ufafanuzi gari lao kubeba wanachama wa CCM

Kusitishwa ufadhili wa Marekani na hatma ya Wafanyakazi wa mashirika Tanzania

TAGGED:Dkt. BitekoPasakaTaifaUchaguzi
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Stellenbosch kuwakosa wakali wawili ikiivaa Simba kombe la Shirikisho
Next Article Video ya mabinti wanaompigania Mwijaku yatua mezani kwa Mhe. Gwajima
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version