Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ametangaza nafasi za za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne wenye sifa mbalimbali ikiwemo kutokutumia madawa ya kulevya, uwezo wa kuongea lugha za kiswahili na kiingereza kwa ufasaha na kutokuwa na alama zozote za kuchorwa mwilini. Maelezo kamili kuhusu tangazo hilo ni kama yafuatayo:-
Taarifa ya Ajira za Jeshi la Polisi
Muajiri : Jeshi la Polisi
Tarehe ya mwisho Kupokea Maombi : 04/04/2025
Nchi : Tanzania
Muhtasari Kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania
Jeshi la Polisi la Tanzania ni moja ya vyombo muhimu vya usalama nchini, linalohusika na kuhakikisha amani, utulivu, na usalama kwa wananchi.
Madhumuni na Majukumu ya Jeshi la Polisi
- Kuhakikisha usalama wa raia na mali zao: Polisi wanawajibika kudumisha utulivu na kuzuia uhalifu katika jamii.
- Kufanya uchunguzi wa uhalifu: Polisi wana jukumu la kuchunguza matukio ya uhalifu na kukusanya ushahidi ili kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.
- Kulinda sheria na amri: Polisi ni chombo cha kutekeleza sheria na amri za serikali.
- Kusaidia na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya usalama: Polisi pia hutoa elimu kuhusu umuhimu wa usalama na sheria.
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I-
- Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.
- Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
- Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8″) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4″) kwa wanawake.
- Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
- Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.
- Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
- Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
- Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
- Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili.
Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania Machi 2025.
Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.
20/03/2025
FANI AMBAZO ZINA NAFASI NI KAMA ZINAVYOONEKANA HAPA CHINI:





JINSI YA KUFANYA MAOMBI KUPITIA MFUMO
Hatua ya 1: Tembelea Tovuti Rasmi ya Jeshi la Polisi
Ili kuanza mchakato wa kutuma maombi, hatua ya kwanza ni kutembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Tovuti hii ni https://ajira.tpf.go.tz/. Hapa utapata taarifa zote zinazohusiana na ajira na jinsi ya kujiunga na Jeshi la Polisi.
Hatua ya 2: Jisajili au Ingia kwenye Mfumo wa Maombi
Baada ya kufungua tovuti, utaona sehemu ya “Ajira”. Bofya hapo ili kupata taarifa zote muhimu kuhusu nafasi za ajira zinazotangazwa. Hapa, utahitaji kujisajili kama mtumiaji mpya au kama tayari una akaunti, unaweza kuingia kwa kutumia jina lako la mtumiaji na nenosiri.
Kwa wale wasio na akaunti:
- Bofya kwenye sehemu ya “Jisajili” na jaza taarifa zako za kibinafsi kama jina, namba ya simu, barua pepe, na taarifa nyingine muhimu.
- Baada ya kujaza taarifa zako, hakikisha unathibitisha usajili wako kwa kufuata maelekezo yatakayokujia kwenye email yako au namba yako ya simu.
Hatua ya 3: Chagua Nafasi ya Ajira
Baada ya kuingia kwenye mfumo, utaona orodha ya nafasi za ajira zinazotolewa na Jeshi la Polisi. Chagua nafasi inayokufaa kulingana na sifa zako na maelezo ya nafasi hiyo.
Hatua ya 4: Jaza Fomu ya Maombi
Hii ni hatua muhimu katika mchakato wa maombi. Utahitaji kujaza fomu ya maombi kwa umakini. Fomu hii inajumuisha:
- Taarifa zako za kibinafsi
- Elimu yako
- Uzoefu wako wa kazi (kama upo)
- Hali yako ya kiafya
- Taarifa za mawasiliano
Hakikisha unajaza kila sehemu ya fomu kwa usahihi na hakikisha taarifa zako ni za kweli. Uongo au taarifa zisizo sahihi zinaweza kupelekea maombi yako kutupiliwa mbali.
Hatua ya 5: Picha na Nyaraka Zilizohitajika
Baada ya kujaza fomu, utahitaji kupakia picha yako ya pasipoti na nakala za nyaraka muhimu kama vile:
- Cheti cha kuzaliwa
- Vyeti vya elimu (vyeti vya kidato cha nne, cha sita, au vyeti vya elimu ya juu)
- Cheti cha afya (ikiwa kinahitajika)
- Nyaraka zingine kama vile vyeti vya uzoefu wa kazi (ikiwa zinahitajika)
Hakikisha picha na nyaraka zako zimepangwa vizuri na zina ubora wa juu ili zisipozuiliwa wakati wa mchakato wa uchambuzi.
Hatua ya 6: Wasilisha Maombi Yako
Baada ya kujaza fomu na kupakia nyaraka zako, hakikisha umetathmini tena maelezo yako yote. Ikiwa kila kitu kiko sawa, bonyeza “Tuma Maombi” ili kuwasilisha maombi yako kwa Jeshi la Polisi.
Hatua ya 7: Subiri Majibu
Baada ya kutuma maombi, utahitaji kusubiri kwa muda ili kujua matokeo. Jeshi la Polisi litawasiliana nawe kupitia namba yako ya simu au barua pepe kwa ajili ya mahojiano au hatua nyingine zinazofuata, kama vile vipimo vya afya au vipimo vya mwili.
Tips Muhimu za Kuzingatia:
Fuatilia Matokeo: Baada ya kutuma maombi, usiache kufuatilia kwa ukaribu ili kujua hatua zinazofuata.
Asanteni kwa taarifa hii njema na nzuri Allah awabariki sana