Pengine umekuwa ukisikia, kusoma na kushuhudia visa na mikasa mbalimbali ya kiimani hapa nchini hivi sasa kiasi cha kujiuliza maswali lukuki kichwani kwamba nini hasa kinatokea kwenye upande huu wa imani za kidini?
Kuanzia manabii wanaoitwa wa uongo au mchongo, tiba za kutoa na kukemea mapepo hadi miujiza ambayo imekuwa ikitangazwa kuwatokea watu karibu kila siku, huku wengine wakiwanyooshea vidole waumini na wengine wahubiri, ilimradi kila mtu ana mtazamo wake.
Lakini katikati ya haya, pengine ni vyema tujikumbushe kwamba mambo haya hayajaanza kutokea leo nchini. Yapo miaka na miaka sasa, lakini kwa mustakabali wa leo, tujikumbushe kuhusu watu waliitwa (au walijiita wenyewe?) Wasabato Masalia.
Mwaka 2008, kuliibuka tukio ambalo litaendelea kubaki kwenye kitabu cha historia ya mambo ya kustaajabisha kuhusiana na imani za kidini nchini Tanzania.
Ni mwaka huo ambako kuliibuka kikundi cha watu ambao siku moja waliamka asubuhi na “misheni” yao ya kutaka kuihubiri Injili ulimwenguni pote. Wakaenda kupiga kambi uwanja wa ndege wa kimataifa Dar-es-salaam, wakisubiri safari yao ya kimiujiza kwenda kuhubiri neno la nchini Iraq na penginepo Duniani.
Waumini hawa, hawakuwa na pasipoti, viza wala tiketi. Hawakufanya mipango yoyote ile ya kusafiri nje ya nchi, walitegemea kusafiri kwa miujiza. Na mpango wao mkubwa ulikuwa ni kufika kule Iraq na Italia na kuhubiri Injili kwa kutumia lugha ya Kiswahili!..Waliamini kwamba kama ilivyotokea siku ya Pentekoste, roho wa Bwana, atashuka, na watu wa Iraq na Italia watakisikia na kukielewa Kiswahili.
Waliamini kwamba wakifika Airport Miujiza itatenda Kazi, watajikuta tu kwenye Ndege za Italia na Iraq na lupaa bila kuulizwa lolote wala Procedures zozote, ukaguzi n.k, Wakakwama!, Safari ikaishia hapo hapo Mitaa ya Kipawa njia panda Jet Rumo, high way ya Gongolamboto.
Haikuwa rahisi wao kukubaliana na hali kwani walibishana sana na Maofisa wa uwanja wa Ndege kwa siku kadhaa wakiwa wamepiga kambi Maeneo Hayo!, Kwamba “Maofisa wa Airport hawalijui neno Wala Maono ya Ki-Ungu.
Waumini 51 wa Dhehebu la Wasabato Masalia, walianzisha kambi katika maeneo ya Tabata baada ya kuzuiwa na kufukuzwa zaidi ya mara 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakita kusafiri kwenda Ulaya kuhubiri Injili bila hati yoyote ya kusafiria huku wakidai wameagizwa na Mungu
Wakiwa Tabata, Waumini hao waliokuwa 17 na kuongezeka hadi 51 walikumbana na hali ngumu ya Maisha, (hivyo kugeuka ombaomba), pia walikuwa wakiugua hawaendi Hospitali kwa kudai “Mungu atawaponya”. Majirani walilalamikia uchafuzi wa Mazingira na kero ya kuombaomba
Inaelezwa Waumini 24 kati yao walihukumiwa kwenda jela Mwaka 1 baada ya kuvamia eneo la watu, lakini hata walipokuwa wakipelekwa gerezani, bado walisema, “Hii ni safari pia na Mungu ana mipango yake.”
Je, hizi ndio zama za mwisho zilizotabiriwa na kutamkwa kwenye vitabu vya dini? Au ni kuchanganyikiwa tu kwa wanaadamu kutokana na msongo wa mawazo au ndio viashiria vya uwepo wa changamoto ya afya ya akili nchini?
Daaah balaaa