By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: Umeme kila mahali ni ndoto ya Rais Samia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Kitaifa

Umeme kila mahali ni ndoto ya Rais Samia

Mwandishi Wetu
Last updated: March 20, 2025 10:06 am
Mwandishi Wetu
2 months ago
Share
SHARE

NAIBU Waziri Judith Kapinga amesema ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona wananchi wote wanapata huduma ya umeme.

Kapinga ameyasema hayo Machi 17, 2025 katika Kijiji cha Mang’oto Wilaya ya Makete mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“Mheshimiwa Rais legacy yake na maono yake ni Tanzania nzima mijini, vijijini na vitongojini kupata umeme, ndio maana mnamuona anahangaika kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya umeme kwenye Vitongoji,” alisema Kapinga.

Aliongeza kuwa, mwaka 2020 Serikali iliahidi kuvifikishia umeme vijiji vyote 12,318 ifikapo Desemba 2025 na wakati Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani takribani Vijiji 4000 havikuwa vimefikiwa na huduma ya umeme.

Katika hatua nyingine Kapinga amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuendelea kutoa ushirikiano kwa wananchi pamoja na utoaji wa elimu wa jinsi ya kufanya maombi ya kuunganisha umeme.

Alitoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa kutumia namba 180 ambayo haina malipo kwa mteja

Kapinga alisisitiza kuwa, azma ya Serikali ni kuhakikisha umeme wa uhakika na unaotabirika unawafikia wananchi wote ili waweze kunufaika kwa shughuli za kiuchumi.

Kufika kwa umeme katika Kijiji cha Mang’oto kumewanufaisha wananchi ambapo wamefungua shughuli za kiuchumi ikiwemo mashine za kusaga nafaka lakini pia kuweza kurahisisha huduma katika Zahanati ya Mang’oto ambayo hapo awali ilikuwa ikitumia umeme wa jua.

Kutokana na hilo wananchi wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa miradi ya umeme Vijijini kwani wameweza kuinua vipato vyao ikiwemo kufungua biashara kama za kuchomelea na kuboresha huduma za afya.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

RC Dar: Usalama Dar ni shwari, Ujenzi Jangwani mboini kuanza

Halotel wazindua huduma kukabili matapeli mitandaoni

Dar msisubiri mwishoni kujiandikisha daftari la wapigakura

Dkt. Samia Suluhu Hassan ampongeza Rais wa Namibia baada ya kuapishwa

Mahakama ya Rufaa yabariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa SSP Bageni

TAGGED:Awamu ya MamaMaendeleoNishatiUmemeUtekelezaji Ahadi
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Ofisi ya Makamu wa Rais yapongezwa
Next Article Bilioni 82.84 zimekopeshwa kwa vijana na wanawake nchini
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version