By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: Bilioni 82.84 zimekopeshwa kwa vijana na wanawake nchini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Kitaifa

Bilioni 82.84 zimekopeshwa kwa vijana na wanawake nchini

Mwandishi Wetu
Last updated: March 20, 2025 10:01 am
Mwandishi Wetu
2 months ago
Share
SHARE

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amesema katika mwaka wa fedha 2024/25, serikali imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 82.84 kwa vikundi 8,275 vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri.

Waziri Mchengerwa ameeleza hayo wakati akiwasilisha mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26 katika vikao vya kamati za kudumu za Bunge linaloendelea jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 40.71 zimetolewa kwa vikundi 4,557 vya wanawake, Shilingi Bilioni 36.64 kwa vikundi 2,827 vya vijana na Shilingi Bilioni 5.48 kwa vikundi 891 vya watu wenye ulemavu.

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeandaa mwongozo wa ukomo wa mkopo ambao utawezesha halmashauri kusimamia utoaji wa mikopo yenye tija kwa jamii na kulingana na mwongozo huo kiwango cha juu cha mkopo kwa kikundi ni Shilingi Milioni 150 na kiwango cha chini cha mkopo ni Shilingi 500,000.

Aidha, Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma imeimarika ambapo upatikanaji wa dawa umeongezeka kutoka asilimia 63.00 mwaka 2023/24 hadi asilimia 79.30 Januari 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.30.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Dk. Kalemani – Sauti ya Wanawake ni Sauti ya Mungu

Kusitishwa ufadhili wa Marekani na hatma ya Wafanyakazi wa mashirika Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa yatahadharisha ongezeko la mvua mwezi Aprili

Polisi Simiyu watoa ufafanuzi gari lao kubeba wanachama wa CCM

Ushirikina wagharimu wagonjwa wa kifafa

TAGGED:Awamu ya MamaMaendeleoMikopoUtekelezaji wa AhadiVijanaWanawake
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Umeme kila mahali ni ndoto ya Rais Samia
Next Article SULEIMAN MATOLA: Tunamchukulia poa poa kwakuwa ni Mtanzania
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version