KOCHA Pitso Mosimane aliamua kumsajili Selemani Matola katika kikosi cha Super Sport ya Afrika Kusini bila ya majaribio.
Katika mahojiano aliyofanya na mwandishi nguli wa habari za michezo nchini, Salehe Ally (Jembe), kocha huyo alisema hakukuwa na haja wakati huo kumjaribu tena Matola sababu mechi mbili Simba Vs Asante Kotoko ya Ghana na Tusker ya Kenya ambao wote walifungwa na Simba katika nusu Fainali na Fainali ya Tusker Cup, Matola alikuwa nyota wa mchezo.
Kwa sasa Matola ni mmoja wa makocha bora wazalendo licha ya kwamba wangeweza kuwa bora zaidi wakishika usukani wa kocha Mkuu.
Matola kajifunza mengi kupitia Simba akiwa msaidizi. Amesimama nyuma ya makocha wa nchi mbali mbali wenye filosofia tofauti na za aina tofauti. Hii inamfanya kuwa bora zaidi.
Licha ya kwamba amekuwa na “damu ya kunguni” Kila Simba ikiyumba anaangushiwa “gari bovu” lakini uhalisia sahihi yeye ni daraja katika ya klabu yake na makocha wa kigeni.
Amekuwa ndiye anayewaelekeza Simba inataka nini, upi ni utamaduni wa maisha ya soka la Simba lakini kwa wachezaji ni Imani naye kubwa na taarifa za uwezo wake kwa kuwa akiwa nahodha aliwahi “kuivua” ubingwa wa Afrika na ubora wa Afrika klabu ya Zamalek, tena kwao jijini Cairo.
Angekuwa si mzawa angeonekana “bonge la kocha”, uzalendo wake umekuwa adhabu lakini amebahatika heri ya subira na kuna siku asipokuwepo Simba watu wengiwatatamani arejee kwa kuwa yeye ni Simba kuanzia jezi yenye jasho uwanjani na sasa ni mapambano kwenye benchi