Utata unaoendelea kuhusu mchezo wa Simba dhidi ya Yanga ulioahirishwa na Bodi ya Ligi Machi 8 kutokana Simba kuzuiliwa kufanya mazoezi, suala hilo linabaki kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na vyombo vyake, kwani serikali haitaki kutia neno.
Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza hayo leo Machi 16 wakati akijibu swali la mwandishi wa habari lililohoji ni upi uamuzi wa serikali kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo.
Akijibu swali hilo mbele ya waandishi wa habari kutokea Bandari Kavu ya Kwala, mkoani Pwani, Msigwa amesema ikitokea TFF wamepeleka suala hilo serikalini basi kwa pamoja watajadili ila kwa sasa serikali haina neno kwa suala lipo kwenye mamlaka zinazohusika.
“Mengine nani alikuwa sahihi na hakuwa sahihi mkawaulize TFF, wao ndio watakuwa na majibu ya jambo hili, lakini sisi kwa sasa serikalini bado tunaona jambo linaweza likatatuliwa na Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) na wadau wake.