By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: Halotel wazindua huduma kukabili matapeli mitandaoni
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
BiasharaKitaifa

Halotel wazindua huduma kukabili matapeli mitandaoni

Mwandishi Wetu
Last updated: March 20, 2025 11:29 am
Mwandishi Wetu
2 months ago
Share
SHARE

Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel imezindua huduma mpya itakayosaidia mteja kujihudumia kwa kutoa taarifa juu ya jambo alilolitilia mashaka ilikupunguza wimbi la utapeli mitandaoni.

Mbali na jambo hilo huduma hiyo pia inatoa nafasi kwa mteja kuangalia Salio, kununua vifurushi na huduma nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Machi 20,2025, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Halotel, Abdallah Salum amesema huduma hiyo inayofahamika kwa jina la ‘Miss Halo’imeziduliwa ili mteja aweze kuwasiliana na kampuni kupitia kitengo cha huduma kwa wateja moja kwa moja.

“Tunajua tulikuwa tukiwasiliana na wateja wetu kupitia namba 100 au mteja kufika ofisini na kueleza shida yake na baadae kutatuliwa,lakini kupitia huduma hii mpya mteja wetu ataweza kujihudumia mwenye bila shida kwani atatumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram pamoja na Whatsapp kwa namba 0620100100,”amesema Salim

“Kwa sasa dunia inaenda kidigitali hivyo na sisi kama kampuni ya mawasiliano ni lazima twende na teknolojia ya kutumia akili mnemba ili kupunguza ama kuondoa kabisa masuala ya utapeli mitandaoni,ni wambie tu wateja wetu huduma hii inazingatia na kutunza taarifa za mteja,”

Amesema kwa sasa sekta ya mawasiliano imekuwa na mageuzi makubwa hivyo ni lazima kuwa na ubunifu na ufanisi hili kuhakikisha wateja wanapata msaada wa haraka na wa kuaminika.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Halotel, Roxana Kadio amesema kampuni hiyo inaendelea kuimarisha sifa yake kama chapa inayojali wateja kwa kutoa sio tu huduma bora za mawasiliano bali uzoefu unaoboresha maisha ya watumiaji wake hivyo jamii itumie huduma hiyo kwani ni rahisi .

Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Halotel, Shaban Said amesema huduma hiyo itaendelea kutatua matatizo ya kawaida na kutoa majibu moja kwa moja na kupunguza muda wa kusubiri kwani imerahisishwa kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Hongera Dkt. Samia Suluhu Hassan, umeweza, tusonge mbele

Ofisi ya Makamu wa Rais yapongezwa

Mbunifu wa jina la TANZANIA afariki dunia akiwa Uingereza

DKT. BITEKO: Wakristo liombeeni Taifa

Bilioni 82.84 zimekopeshwa kwa vijana na wanawake nchini

TAGGED:BiasharaHalotelMitandaoUtapeli
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Wananchi Mtwara wawaelimishwe kuhusu uchaguzi mkuu – Padri Kitima
Next Article Dar msisubiri mwishoni kujiandikisha daftari la wapigakura
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version