Shauri la mapitio ya hukumu ya kunyongwa iliyokuwa imetolewa kwa SSP Christopher Bageni, limetamatika kwa mahakama ya rufaa nchini kuafiki hukumu hiyo ambayo ilitolewa na mahakama hiyo hiyo miaka 9 iliyopita.
Uamuzi huo ulitolewa februari 19, 2025 na Jani Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo na kwa uamuzi huo SSP Bageni sasa hawezi tena kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya jana imetolewa baada ya ni mapitio (review) ya hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda.
Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.
Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Mhe. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.
Zombe alifanikiwa “kuchomoka” kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na maamuzi yakasomwa jana kuwa anyongwe hadi kufa