WADAU mbalimbali katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wameiomba serikali kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendeleza jitihada za kutoa elimu kuhusu vitendo vya ukatili ya kijinsi vinayoendelea kwenye jamii yao.
Haya yamejiri wakati wa kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi kwenye manispaa hiyo kuhusu kukumbushana na masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo ardhi, ndoa, talaka, ukatili wa kijinsia kwa wanawake, watoto na makundi maalumu ili kila mmoja aendelee kuwa balozi wa kufikisha elimu hiyo kwa jamii.
Kikao hicho kimefanyika kwenye manispaa hiyo, kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali linachojishughulisha na utoaji wa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto (NERIO) lililopo katika Manispaa hiyo kupitia mradi wa Sauti ya Mwanamke.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa mtaa wa pentekosti, Hassan Mtiko amesema elimu hiyo ni muhimu katika jamii yao kutokana vitendo hiyo vipo kwenye jamii yao na kuziomba taasisi zinazohusika na masuala ya kisheria kuendelea kutoa ushirikiano wanapopelekewa taarifa za kuwepo kwa vitendo hivyo .
Mshiriki mwingine wa kikao hicho, Zainabu Kibunju mkazi wa kata ya mitengo ‘’Niwaombe wanawake wenzangu waache vitendo vya ukatili kwa wanaume hasa wale wanaojishughulisha na vitendo hivi kwa wanaume zao na wanaume nao waache kufanya vitendo hivi kwa wanawake zao na tunaiomba serikali, wadau elimu hii ifike zaidi katika jamii yetu’’
Mratibu wa Shirika hilo la NERIO Saidi Ismail amesema lengo la kikao hicho ni kukumbusha juu ya masuala hayo ya kisheria ili kila mmoja kwa nafasi yake aendelee kupaza sauti kuhusu vitendo hiyo vya ukatatili inavyoendelea kwa wanaume, wanawake na watoto kwenye jamii hiyo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwenye manispaa hiyo, Juliana Manyama amezitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa kesi za namna hiyo zinapofika kwao zifanyiwe kazi kwa haraka ziishe na ifike mahali vitendo hivyo viishe kabisa.

‘’Tunalo jukumu kila mmoja kwa nafasi yake tujue inafikia mahali iwe mwisho wa vitendo hivi na haviwezekani kufikiwa na taasisi moja pekee bali ni jukumu la kila mtu’’amesema Manyama