By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: Hakikisheni elimu ya malezi inaifikia jamii kikamilifu – Theresia Ngonyani
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Mikoani

Hakikisheni elimu ya malezi inaifikia jamii kikamilifu – Theresia Ngonyani

Mwandishi Wetu
Last updated: February 20, 2025 9:19 am
Mwandishi Wetu
3 months ago
Share
SHARE

WATENDAJI katika Halmashauri mbalimbali mkoani Mtwara wametakiwa kuhakikisha elimu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inafikia kikamilifu kwa jamii pamoja na wadau kwa ujumla.

Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa shughuli za Programu Jumuishi ya Taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) Mkoa wa Mtwara kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024, uliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kukutanisha watendaji hao pamoja na wadau.

Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Theresia Ngonyani amesema elimu hiyo iende kwa kila mtu, mdau ili kwa pamoja waweze kulea watoto wao katika ukuaji uliyotimilika ili mwisho wa siku wawe na wananchi au raia waliyokuwa wema wanaofanya matendo mema pasipo kuwepo mmomonyoko wa maadili.

‘’Halmashauri kupitia kwa waratibu na waratibu wengine katika maeneo matano ya mpango huu wa MMMAM kuweza kuifikia jamii wanayotoka wao wenyewe katika halmashauri zao kuanzia ngazi ya kijiji, mtaa, kata pamoja na halmashauri elimu hii iweze kwenda kwa kila mtu na wadau kwa ujumla’’amesisitiza Ngonyani

Aidha katika malengo ya mpango huo waliyojiwekea watendaji hao ya kuhakikisha wanazifikia shule za awali pamoja na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana (Baby Cares), wahakikishe wanafikia malengo husika ya mpango kwa kuwafikia walengwa ambao ni mtoto kuanzia mwaka 0 hadi miaka 8.  

Meneja Uchechemuzi wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto Nchini (TECDEN), Bruno Ghumpi amesema watoto chini ya miaka mitano nchini asilimia 47 wako kwenye ukuaji wao sahihi na asilimia 53 hawako kwenye ukuaji sahihi hali inayowafanya wawekeze zaidi kwenye eneo hilo.

‘’Kwa hali hii inatufanya kuwekeza zaidi kama taifa ili tuwapate hawa watoto wawe na tija kwa taifa, wawe ni watu wenye afya njema, uelewa na wanaoweza kukafanya kazi za uzalishaji’’ amesema Bruno

Mkurugenzi wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (MTWANGONET) mkoani humo, Fidea Luanda ametoa ushauri kwa watendaji hao kuwa kwenye mikutano hiyo kuwe na utaratibu unaoruhusu kuwataja watoto wenye mahitaji maalumu kama iliyokuwa watoto wengine ili kuzingatia usawa katika elimu hiyo.

Mwenyekiti wa Baby Cares Mkoa wa Mtwara, Selemani Mkonga amewaomba watendaji hao kuwa pale wanapofanya mikutano yao na wazazi katika shule hizo ni vema  wakashirikisha vituo hivyo vya baby cares ili kuboresha zaidi  utaoji wa elimu hiyo na mkoa una jumla ya baby cares 180.

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Wapeni wake zenu nafasi ya kuendeleza ujuzi wao

Wananchi Mtwara wawaelimishwe kuhusu uchaguzi mkuu – Padri Kitima

Madiwani Tandahimba wapitisha bajeti ya bilioni 40.2

Polisi Simiyu watoa ufafanuzi gari lao kubeba wanachama wa CCM

Mhe. Kanyasu atimiza ahadi ya pikipiki kwa wanahabari Geita

TAGGED:ElimuMtwaraWatendaji
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Madiwani Tandahimba wapitisha bajeti ya bilioni 40.2
Next Article Geita yafikia 95% utekelezaji wa ilani ya CCM
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version