By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
YanayojiriYanayojiriYanayojiri
  • Home
  • Home
    • Home 2
    • Home 3Hot
    • Home 4
    • Home 5New
  • Posts
    • Post Layouts
    • Gallery Layouts
    • Video Layouts
    • Audio Layouts
    • Post Sidebar
    • Review
      • User Rating
    • Content Features
    • Table of Contents
  • Pages
    • Search Page
    • 404 Page
Reading: AJALI ZA BARABARANI ZINACHANGIA ASILIMIA 55 YA WANAOLIPWA FIDIA WCF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
YanayojiriYanayojiri
Font ResizerAa
  • Categories
  • Home
    • Home 1
    • Home 2
    • Home 3
    • Home 4
    • Home 5
  • More Foxiz
    • Login
    • Contact
    • Blog
    • Buy Theme
  • Demos
  • Categories
  • Bookmarks
  • More Foxiz
    • Sitemap
Have an existing account? Sign In
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Kitaifa

AJALI ZA BARABARANI ZINACHANGIA ASILIMIA 55 YA WANAOLIPWA FIDIA WCF

Baadhi ya washiriki wa matembezi ya kuadhimisha wiki ya kimataifa ya usalama barabarani yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Mwandishi Wetu
Last updated: May 19, 2025 10:29 am
Mwandishi Wetu
1 week ago
Share
SHARE

Karibu asilimia 55 ya taarifa za vifo vinavyoripotiwa katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini (WCF) ni zile zinazoonyesha kuwa chanzo chake ni ajali za barabarani, takwimu zinazoashiria kuwa ajali hizo ni janga lenye kugharimu nguvu kazi ya taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar, katika hafla fupi ya kuhitimisha maadhimisho ya nane ya Wiki ya Kimataifa ya Usalama Barabarani iliyoandaliwa na asasi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA Tanzania) na kufadhiliwa na mfuko huo pamoja na Shirika la Kimataifa la Global Alliance.

Akiongea mbele ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo, Dkt. Omar amesema, takwimu hizo mbali ya kudhoofisha nguvu kazi katika kukuza uchumi wa nchi, zinaonyesha ni kwa kiasi gani mfuko huo unatakiwa kuwekeza katika kushirikiana na wadau kwenye jitihada za kuimarisha usalama barabarani nchini.

Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa WCF Dkt. Omar akiongea na washiriki wa matembezi hayo katika ufukwe wa Coco, yalikotamatikia matembezi.

“Ushiriki wetu katika tukio hili unaendelea kuonyesha azma ya WCF ya kuimarisha na kuendeleza ushirikiano wetu na wadau katika kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inafika kwa watumiaji wote wa barabara pamoja na kuhamasisha watumia barabara hao kupaza sauti ili kwa pamoja tutokomeze ajali hizi ambazo ni mzigo kwa taifa letu” amesema Dkt. Omar.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa huduma za Tathmini wa WCF, ameendelea kusisitiza wafanyakazi wanaopata ajali wakiwa njiani kwenda au kutoka makazini au wakiwa katika safari za kikazi, kuhakikisha wanawasiliana na mfuko huo, kwani hao ni wenye kustahili kulipwa fidia kupitia mfuko huo.

Akiongea katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa RSA Tanzania balozi Augustus Fungo amesema, Shirika linajivunia kuwa asasi kinara katika harakati za kuimarisha usalama barabarani nchini kupitia programu mbalimbali za uelimishaji, ukemeaji na utoaji taarifa za changamoto za barabarani, na kuwashukuru wadau wote ambao wamekuwa wakijitokeza kuunga mkono juhudi hizo wanazozifanya.

“Asasi hii inaundwa na watu ambao wanajitolea kwa zaidi ya asilimia 90, wakijitolea muda na gharama zao ili kutekeleza programu za taasisi, licha ya uhaba wa vitendea kazi kama vipeperushi kwa ajili ya uelimishaji na hata kufanya machapisho mengine yenye lengo la kuelimisha na tunaomba wadau waendelee kutuunga mkono kwa kuwa usalama barabarani ni jukumu letu sote.

Maadhimishi ya nane ya Wiki ya Kimataifa ya Usalama Barabarani 2025, yalibeba ujumbe wa Tuimarishe Usalama wa Watembea kwa Miguu na Waendesha Baiskeli, ujumbe ambao umelenga kuhamasisha mamlaka zinazohusika na usanifu na ujenzi wa barabara kuhakikisha zinajumuisha miundombinu kwa ajili ya kundi hilo la watumia barabara, ambalo limekuwa likiathiriwa zaidi na matukio ya ajali za kugongwa na vyombo vya moto.

Baadhi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani wakiwa katika matembezi ya maadhimisho hayo
Maadhimisho ya Mwaka Huu yalikuwa na ujumbe wa kuwalinda watembea kwa miguu na waendesha baiskeli

Share this:

  • Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
  • Click to share on X (Opens in new window) X

You Might Also Like

Umeme kila mahali ni ndoto ya Rais Samia

Dk. Kalemani – Sauti ya Wanawake ni Sauti ya Mungu

Rais Samia aagiza madereva wanaosababisha vifo kufutiwa kabisa leseni zao

DKT. BITEKO: Wakristo liombeeni Taifa

Ofisi ya Makamu wa Rais yapongezwa

TAGGED:8UNRSWRSA TanzaniaWCF
Share This Article
Facebook Email Print
Previous Article Mkuu wa Wilaya Ubungo ateuliwa Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Leave a Comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

UNGANA NASI

Unaweza kuwa sehemu ya familia hii kwa kuchangia kuleta taarifa za yanayojiri eneo lako, kuchangia makala, kushirikisha uzoefu wako kwa kutoa maoni na hata kuuliza ili kufahamu zaidi. Kujiunga nasi, tafadhali tuandikie kupitia karibu@yanayojiri.com  

© Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Join Us!
Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..
Zero spam, Unsubscribe at any time.
Go to mobile version